Al-An'aam 6:131
الأنعامذَٰلِكَ أَن لَّمْ يَكُن رَّبُّكَ مُهْلِكَ ٱلْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا غَـٰفِلُونَ
Hayo ni kwa sababu ya kuwa Mola wako Mlezi hakuwa ni wa kuiangamiza miji kwa dhuluma, hali ya kuwa wenyewe wameghafilika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hayo ni kwa sababu ya kuwa Mola wako Mlezi hakuwa wa kuiangamiza miji kwa dhulma, hali wenyewe wameghafilika. [131]
[131] Na huku kutuma Mitume, wenye kuonya na kubainisha ni kwa kuwa Mola wako Mlezi, ewe Nabii, haiangamizi miji kwa dhulma yao na watu wake wameghafilika na Haki tu. Bali hapana budi ila awabainishie kwa uwazi na awaonye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ili asiadhibiwe yoyote kwa kujidhulumu nafsi yake kwa kufanya maovu na hali ulinganizi wa Uislamu haujamfikia, sisi tulituma Mitume na tukateremsha Vitabu kwa kuwaondolea majini na binadamu hoja watakayoichukua kama kisingizio. Hivyo ndivyo tulivyowaondolea hoja umma waliopita, hatukumuadhibu yoyote isipokuwa baada ya kuwapelekea Mitume.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net