Al-An'aam 6:132
الأنعاموَلِكُلٍّ دَرَجَـٰتٌ مِّمَّا عَمِلُوا۟ ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ
Na kila mmoja ana daraja mbalimbali kutokana na yale waliyoyatenda. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika mbali na yale wanayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wote wana daraja mbali mbali kutokana na yale waliyo yatenda. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na yale wanayo yatenda. [132]
[132] Na kila mtenda kheri au mtenda shari ana daraja yake ya malipo kwa anayo yatenda. Ikiwa kheri atapata kheri, na ikiwa shari basi atapata shari. Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika ndiye Muumba, si Mwenye kughafilika na wanayo yatenda. Bali hakika vitendo vyao vimo katika Kitabu kisicho acha dogo wala kubwa ila hulitia hisabuni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kila mwenye kufanya vitendo vya kumtii Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na vya kumuasi ana daraja kutokana na vitendo vyake, Allah Mtukufu Atamfikishia viwango hivyo na Atamlipa kwavyo. Na Mola wako, ewe Mtume, Hakuwa ni Mwenye kughafilika na wanayoyafanya waja Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net