Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 133

Al-An'aam 6:133

الأنعام

وَرَبُّكَ ٱلْغَنِىُّ ذُو ٱلرَّحْمَةِ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَسْتَخْلِفْ مِنۢ بَعْدِكُم مَّا يَشَآءُ كَمَآ أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوْمٍ ءَاخَرِينَ

Maana

Na Mola wako Mlezi ndiye asiyemhitaji yeyote, Mwenye rehema. Akitaka, atawaondoa na awaweke nyuma yenu wengine awatakao, kama vile alivyokutoeni kutokana na dhuria ya kaumu wengine.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mola wako Mlezi ndiye Mkwasi, Mwenye rehema. Akipenda atakuondoeni na awaweke wengine awapendao badala yenu, kama vile alivyo kutoeni kutokana na uzazi wa watu wengine. [133]

[133] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mola wako Mlezi, ni Mkwasi, hahitajii waja wala ibada zao. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye rehema iliyo kusanya kila kitu. Na kwa mujibu wa hayo ndio akakuamrisheni mtende mema, na akakukatazeni maovu. Naye ndiye Muweza. Akitaka atakuondoeni na alete duniani wenginewe wa kufuatia baada yenu kwa mujibu wa atakavyo. Wala hilo si gumu kwake Subhanahu, Aliye takasika. Kwani Yeye alikuumbeni kutokana na uzao wa wengine walio kutangulieni. Nanyi mkawa ndio warithi wa ardhi baada yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Mola wako, ewe Mtume, Aliyewaamrisha watu kumuabudu, Ndiye Mkwasi Peke Yake, na viumbe wote wanamhitajia Yeye. Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Mwenye rehema kunjufu. Na lau angetaka Angaliwaangamiza na Akawaleta watu wengine wasiokuwa nyinyi watakaokuwa badala yenu baada ya kumalizika kwenu na watende matendo ya kumtii Yeye, Aliyetukuka, kama Alivyowaleta nyinyi kutokamana na kizazi cha watu wengine waliokuwako kabla yenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net