Al-An'aam 6:134
الأنعامإِنَّ مَا تُوعَدُونَ لَـَٔاتٍ ۖ وَمَآ أَنتُم بِمُعْجِزِينَ
Hakika, yale mnayoahidiwa yatafika, wala nyinyi hamtaweza kushinda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Bila ya shaka hayo mnayo ahidiwa yatafika tu, wala nyinyi hamtaweza kuyaepuka. [134]
[134] Na hayo anayo kuonyeni kwayo, nayo ni adhabu, na anayo kubashirieni kwayo, nayo ni thawabu baada ya kufufuliwa, na kukusanywa, na kuhisabiwa, yatakuja tu hapana hivi wala hivi. Wala nyinyi hamwezi kumshinda huyo anaye kutakeni Siku hiyo. Basi hamna uwezo wa kukataa kukusanyika wala kuhisabiwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika yale mateso ambayo Anawaahidi nayo Mola wenu, enyi washirikina, kwa ukafiri wenu, ni yenye kuwapata. Na hamtamlemea Mola wenu kwa kumkimbia. Kwani Yeye ana uwezo wa kuwarudisha, hata kama mtakuwa mmegeuka mmekuwa mchanga na mifupa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net