Al-An'aam 6:135
الأنعامقُلْ يَـٰقَوْمِ ٱعْمَلُوا۟ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّى عَامِلٌ ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُۥ عَـٰقِبَةُ ٱلدَّارِ ۗ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلظَّـٰلِمُونَ
Sema: Enyi kaumu yangu! Fanyieni pahali penu mlipo, na hakika mimi ninafanya. Mtakuja jua ni ya nani yatakuwa makazi mema mwishoni. Hakika, madhalimu hawafaulu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Enyi watu wangu! Fanyeni muwezayo, na hakika mimi nafanya. Mtakuja jua nani atakuwa na makaazi mema mwishoni. Hakika madhaalimu hawatafanikiwa. [135]
[135] Ewe Nabii! Waambie kwa kuwatisha: Fanyeni kama mpendavyo kwa ukomo wa uwezo wenu. Na mimi nitafanya kwa mujibu wa Haki. Na mwishoe bila ya shaka mtajua nani atakuwa na khatima njema katika makaazi ya Akhera. Na hayo watayapata watu wa Haki, hapana hivi wala hivi. Kwa sababu nyinyi ni madhaalimu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwaandikia kufuzu walio dhulumu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, «Enyi watu wangu, fanyeni kwa njia yenu, na mimi nitafanya kwa njia yangu ambayo Mola wangu, Aliyetukuka na kuwa juu, Aliniwekea. Mtakuja kujua, pindi mateso yatakapowashukia, ni nani atakayekuwa na mwisho mwema?» Hakika hatafaulu kupata radhi za Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na Pepo yule aliyekiuka mpaka Wake na akadhulumu, na akamshirikisha pamoja na Allah Mtukufu asiyekuwa Yeye.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net