Al-An'aam 6:136
الأنعاموَجَعَلُوا۟ لِلَّهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ ٱلْحَرْثِ وَٱلْأَنْعَـٰمِ نَصِيبًا فَقَالُوا۟ هَـٰذَا لِلَّهِ بِزَعْمِهِمْ وَهَـٰذَا لِشُرَكَآئِنَا ۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَآئِهِمْ فَلَا يَصِلُ إِلَى ٱللَّهِ ۖ وَمَا كَانَ لِلَّهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَآئِهِمْ ۗ سَآءَ مَا يَحْكُمُونَ
Na walimwekea Mwenyezi Mungu fungu katika mimea na wanyama alioumba, wakasema: 'Hii ni sehemu ya Mwenyezi Mungu - kwa madai yao - na hii ni ya washirikishwa wetu.' Basi vile vilivyokuwa vya washirikishwa wao, havimfikii Mwenyezi Mungu, vile vilivyokuwa vya Mwenyezi Mungu, huwafikia washirikishwa wao. Ni uovu mno hayo wanayoyahukumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wamemwekea sehemu Mwenyezi Mungu katika mimea na wanyama alio umba, nao husema: Hii ni sehemu ya Mwenyezi Mungu - kwa madai yao - na hii ni ya miungu tunao washirikisha. Basi vile walivyo wakusudia miungu yao havimfikii Mwenyezi Mungu, na vilivyo kuwa vya Mwenyezi Mungu huwafikia miungu yao. Ni uovu kabisa hayo wanayo yahukumu. [136]
[136] Na washirikina, ambao wanayaabudu masanamu, wamo katika udanganyifu wa daima. Wao hufanya katika aliyo yaumba Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika mazao ya mimea, na ngamia, na ng'ombe, na kondoo, fungu la Mwenyezi Mungu Mtukufu wakiwatumilia wageni na wenye haja, na fungu jingine hulitumia katika kuwakhudumia masanamu ambayo wameyafanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa mujibu wa madai yao! Ama walicho wawekea masanamu huwafikia masanamu yao, na hukitumia kwa ajili yao. Na walicho muwekea Mwenyezi Mungu Mtukufu hakifiki chochote kwa hao wageni na mafakiri! Uovu ulioje huu wa hukumu yao ya dhulma! Kwani wao wameyafanya masanamu ndio wenziwe Mwenye kuumba hiyo mimea na wanyama, na hawatumii inavyo stahiki hicho walicho mwekea Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale wenye kumshirikisha Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, waliziweka kando sehemu ya vitu Alivyoviumba miongoni mwa mazao, matunda na wanyama howa wakawapatia wageni na maskini; na wakaziweka kando sehemu nyingine za vitu hivi kwa washirika wao, miongoni mwa masanamu na mizimu. Basi zile zilizotengewa washirika wao zafikishwa kwao peke yao, na hazifiki kwa Allah Mtukufu; na zile zilizotengewa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, zinafika kwa washirika wao. Ni mbaya ulioje uamuzi wa hao watu na kigawanyo chao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net