Al-An'aam 6:128
الأنعاموَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا يَـٰمَعْشَرَ ٱلْجِنِّ قَدِ ٱسْتَكْثَرْتُم مِّنَ ٱلْإِنسِ ۖ وَقَالَ أَوْلِيَآؤُهُم مِّنَ ٱلْإِنسِ رَبَّنَا ٱسْتَمْتَعَ بَعْضُنَا بِبَعْضٍ وَبَلَغْنَآ أَجَلَنَا ٱلَّذِىٓ أَجَّلْتَ لَنَا ۚ قَالَ ٱلنَّارُ مَثْوَىٰكُمْ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ
Na ile Siku atakapowakusanya wote, “Enyi kundi la majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanadamu.” Na marafiki zao katika wanadamu watasema: 'Mola wetu Mlezi! Tulinufaishana baadhi yetu kwa wenzi wetu, na tumefikia muda wetu uliotuwekea.' Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndiyo makazi yenu, mtadumu humo, isipokuwa apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hekima, Mwenye kujua zaidi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ile Siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu. Na marafiki zao katika wanaadamu waseme: Mola Mlezi wetu! Tulinufaishana sisi na wao. Na tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea. Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makaazi yenu, mtadumu humo, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hikima, na Mwenye kujua. [128]
[128] Na ilivyo kuwa wale walio ifuata Njia ya Mwenyezi Mungu Iliyo Nyooka watapata amani na ulinzi wa Mwenyezi Mungu, basi wale walio ifuata njia ya Shetani watapata malipo ya maasi waliyo yafanya hapo watapo kusanywa wote Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu Aliye tukuka kwa Utukufu wake atawaambia hao majini na watu walio tenda dhambi: Enyi mlio kusanyika, katika majini hadi mmekithiri kuwapoteza watu, hata wamekufuateni wengi! Tena watasema wale watu walio wafuata: Ewe Muumba wetu na Mwenye kutusimamia! Hakika sisi kwa sisi tulipeana manufaa, na tukapeana starehe kwa matamanio; na sasa ajali yetu uliyo tuwekea imekwisha fika. Hapo Mwenyezi Mungu Aliye tukuka kwa utukufu wake atasema: Makaazi yenu ya kukaa ni Motoni. Mtadumu humo milele, isipo kuwa Mwenyezi Mungu atakao penda kuwavua katika wale wasio kanya Ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Na hakika vitendo vya Mwenyezi Mungu daima vinakuwa kwa mujibu wa hikima na ujuzi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka, ewe Mtume, ile Siku Atakayowakusanya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, makafiri na wategemewa wao, miongoni mwa mashetani wa kijini, na kuwaambia, «Enyi mkusanyiko wa majini, hakika mumewapoteza binadamu wengi.» Na watasema wategemewa wao miongoni mwa makafiri wa kibinadamu, «ewe mola wetu, kila mmoja katika sisi amenufaika na mwingine, na tumefikia kikomo ambacho umekiweka kwetu kwa kumalizika uhai wetu wa duniani.» Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Atasema Awaambie, «Moto ndio mashukio yenu, mtakaa milele, isipokuwa yule ambaye Allah Mtukufu Ametaka asikae milele,» miongoni mwa walioasi wenye kumpwekesha Allah Mtukufu. Hakika Mola wako ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake na utengenezaji Wake, ni Mjuzi mno wa mambo yote ya waja Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net