Al-An'aam 6:127
الأنعاملَهُمْ دَارُ ٱلسَّلَـٰمِ عِندَ رَبِّهِمْ ۖ وَهُوَ وَلِيُّهُم بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
Hao watapata nyumba ya salama kwa Mola wao Mlezi. Naye ndiye Rafiki Mlinzi wao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao watapata nyumba ya salama kwa Mola Mlezi wao. Naye ndiye Rafiki Mlinzi wao kwa sababu ya waliyo kuwa wakiyatenda. [127]
[127] Na hawa wanao kumbuka na wanao amini watapata Nyumba ya Amani, nayo ndiyo Pepo. Nao watakuwa chini ya ulinzi na urafiki wa Mwenyezi Mungu na mapenzi yake na nusra yake, kwa sababu ya mambo ya kheri waliyo yatenda duniani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale wanaokumbuka watapata mbele ya Mola wao, Aliyetukuka na kuwa juu, Siku ya Kiyama Nyumba ya Salama na Amani, isiyo na makero, nayo ni Pepo. Na yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ni Mwenye kuwanusuru na kuwalinda; hayo yakiwa ni malipo kwao kwa matendo yao mema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net