Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 126

Al-An'aam 6:126

الأنعام

وَهَـٰذَا صِرَٰطُ رَبِّكَ مُسْتَقِيمًا ۗ قَدْ فَصَّلْنَا ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ

Maana

Na hii ndiyo Njia ya Mola wako Mlezi iliyonyooka. Tumeshazieleza Aya kwa kina kwa kaumu wanaokumbuka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hii ndiyo Njia ya Mola wako Mlezi Iliyo nyooka. Tumezipambanua Aya kwa watu wanao kumbuka. [126]

[126] Na hii tuliyo ibainisha ndio Njia ya Haki Iliyo Nyooka. Nasi tumeipambanua na tumeiweka wazi kwa watu wote, na wala hawanufaiki kwayo ila wale ambao shani yao ni kukumbuka na kutaka hidaya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na haya tuliyokubainishia, ewe Mtume, ndio njia inayofikisha kwenye radhi za Mola Wako na Pepo Yake. Tumezifunua wazi hoja kwa yule anayekumbuka miongoni mwa wenye akili zilizokomaa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net