Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 125

Al-An'aam 6:125

الأنعام

فَمَن يُرِدِ ٱللَّهُ أَن يَهْدِيَهُۥ يَشْرَحْ صَدْرَهُۥ لِلْإِسْلَـٰمِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُۥ يَجْعَلْ صَدْرَهُۥ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِى ٱلسَّمَآءِ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْعَلُ ٱللَّهُ ٱلرِّجْسَ عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ

Maana

Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumuongoa, humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule anayetaka kumpoteza, hukifanya kifua chake kuwa na dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda katika mbingu kwa ugumu mkubwa. Namna hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anaweka uchafu juu ya wale wasioamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumhidi humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na anaye taka apotee hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda mbinguni. Namna hivi Mwenyezi Mungu anajaalia uchafu juu ya wasio amini. [125]

[125] Ikiwa hao wamepotea, na nyinyi mkaongoka, basi ni kwa kutaka Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa hukumu yake. Aliye muandikia hidaya humkunjulia kifua chake kwa nuru ya Uislamu. Na aliye muandikia kupotea kifua chake huwa na dhiki ya kweli kweli, kama kinavyo mbana kifua mwenye kupanda pahala pa juu, kama vile mbinguni. Pumzi humpaa, asiweze kitu! Na kwa hivi Mwenyezi Mungu huwaandikia ufisadi na kukatika tamaa hao ambao hawakujaaliwa kuwa na Imani katika shani yao. Masomo ya ilimu za sayansi yamethibitisha kuwa mwanaadamu kila akipanda juu kunadhoofika kuvuta pumzi kwake kwa pua. Mpaka akifika mnyanyuka wa futi 12,000 huwa hawezi kuvuta kwa pua, na huvuta pumzi kwa mdomo. Na hivyo huvuta kwa shida, na akifanya juhudi yoyote ya nguvu huzidi taabu ya kuvuta pumzi. Na hata kusema humletea shida katika pumzi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi yule ambaye Allah Mtukufu Anataka kumuafikisha aikubali haki, Anakikunjua kifua chake kukubali Imani na upweke wa Allah Mtukufu; na yule ambaye Anataka kumpoteza, Anakifanya kifua chake kiwe katika hali ya dhiki kubwa na kukunjika katika kuukubali uongofu, kama hali ya anayepaa kwenye tabaka za anga za juu, hapo akapatwa na uzito mkubwa wa kuvuta pumzi. Na kama anavyovifanya Allah Mtukufu vifua vya makafiri vibanike sana na kukunjika, hivyo basi ndivyo Atakavyowapatia adhabu wale wasiomuamini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net