Al-An'aam 6:124
الأنعاموَإِذَا جَآءَتْهُمْ ءَايَةٌ قَالُوا۟ لَن نُّؤْمِنَ حَتَّىٰ نُؤْتَىٰ مِثْلَ مَآ أُوتِىَ رُسُلُ ٱللَّهِ ۘ ٱللَّهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُۥ ۗ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ أَجْرَمُوا۟ صَغَارٌ عِندَ ٱللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌۢ بِمَا كَانُوا۟ يَمْكُرُونَ
Na inapowajia Ishara, wao husema: 'Hatutaamini mpaka tupewe mfano wa yale waliyopewa Mitume wa Mwenyezi Mungu.' Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi ni wapi anaweka ujumbe wake. Itawafikia wale waliofanya uhalifu udhalili kwa Mwenyezi Mungu, na adhabu kali kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na inapo wajia Ishara, wao husema: Hatutoamini mpaka tupewe mfano wa walio pewa Mitume wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake. Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya. [124]
[124] Hakika hawa wakuu wa wakosefu huwahusudu watu walio pewa na Mwenyezi Mungu ilimu, na Unabii, na uwongofu. Basi ikiwajia hoja ya kukata hawaikubali, lakini husema: Hatuikubali Haki mpaka tuteremshiwe wahyi kama wanavyo teremshiwa Mitume. Na hali ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye ujuzi ambao haulingani na ujuzi wa mtu yoyote, kujua nani anaye stahiki kupata Utume wake. Ni Yeye ndiye anaye teuwa nani katika viumbe vyake ampe Utume wake. Hawa wenye inda, ikiwa wanataka ukubwa kwa inadi ya namna hii, basi watakuja pata unyonge na udhalili hapa duniani kwa sababu hiyo, na kesho Akhera watakuja pata adhabu kali kwa sababu ya huko kupanga kwao uwovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na pindi inapowajia washirikina hawa, miongoni mwa watu wa Maka, hoja iliyo waziwazi juu ya unabii wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,) wanasema baadhi ya wakubwa wao, «Kamwe hatutaukubali unabii wake mpaka Allah Mtukufu Atupe unabii na miujiza mfano wa Aliyowapa wajumbe wake waliotangulia» Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Aliwajibu kwa neno lake,: «Allah Mtukufu Anajua zaidi wapi Auweke ujumbe Wake.» Kwa maana kuwa Anawajua wale wanaofaa kubeba ujumbe Wake na kuufikisha kwa Watu. Utawapata unyonge wakiukaji mipaka hawa, na watakuwa na adhabu iumizayo ndani ya Moto wa Jahanamu kwa sababu ya vitimbi vyao kwa Uislamu na watu wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net