Al-An'aam 6:123
الأنعاموَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا فِى كُلِّ قَرْيَةٍ أَكَـٰبِرَ مُجْرِمِيهَا لِيَمْكُرُوا۟ فِيهَا ۖ وَمَا يَمْكُرُونَ إِلَّا بِأَنفُسِهِمْ وَمَا يَشْعُرُونَ
Na namna hivi tumeweka katika kila mji wakubwa wa wahalifu ili wafanye vitimbi ndani yake. Na wala hawafanyii vitimbi isipokuwa nafsi zao ilhali hawatambui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kadhaalika katika kila mji tumewajaalia wakubwa wa wakosefu wao wafanye vitimbi ndani yake. Na wala hawafanyii vitimbi isipo kuwa nafsi zao, nao hawatambui. [123]
[123] Ewe Nabii! Usistaajabu ukiwaona wakuu wa wakosefu katika Makka wanapanga njama za shari za kila namna! Kwani huo ndio mtindo wao katika kila mji mkubwa. Wakuu wa wakosefu wake huwa kazi yao kuzua vitimbi vya shari. Na malipo ya uovu wake utakuja waangukia wenyewe, lakini wao hawatambui wala hawahisi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mfano huu uliopatikana kwa viongozi wa makafiri huko Maka wa kuzuia dini ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, tumeweka katika kila mji watu waovu wanaongozwa na wakubwa wao, ili wapate kufanya vitimbi humo kwa kuzuia dini ya Allah Mtukufu; na wao hawazifanyii vitimbi isipokuwa nafsi zao, na wala hawalihisi hilo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net