Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 122

Al-An'aam 6:122

الأنعام

أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَـٰهُ وَجَعَلْنَا لَهُۥ نُورًا يَمْشِى بِهِۦ فِى ٱلنَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُۥ فِى ٱلظُّلُمَـٰتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْكَـٰفِرِينَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Maana

Je, yule aliyekuwa maiti, kisha tukamhuisha, na tukamfanyia nuru akatembea kwayo katika watu, ni kama yule ambaye mfano wake yuko katika giza mbalimbali, sio wa kutoka humo? Kama hivyo ndivyo makafiri walivyopambiwa yale waliyokuwa wakiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je, aliye kuwa maiti kisha tukamhuisha, na tukamjaalia nuru inakwenda naye mbele za watu, mfano wake ni kama aliyoko gizani akawa hata hawezi kutoka humo? Kama hivyo makafiri wamepambiwa waliyo kuwa wakiyafanya. [122]

[122] Na nyinyi kwa Imani yenu si mfano wa washirikina hata kidogo. Basi haiwezi kuwa hali ya aliye kama maiti katika kupotea kwake, na Mwenyezi Mungu akampa nuru ya kuhidika, ambayo ni kama uhai, na akampa nuru ya Imani na hoja zilizo wazi, na kwa mwangaza wa nuru hiyo akaongoka na akawa anatembea nayo, haiwezi kuwa hali hiyo mfano wa hali ya ambaye kwamba anaishi katika giza lilio gubika. Na kama Mwenyezi Mungu alivyo ipamba Imani katika nyoyo za watu wa Imani, vile vile Shetani ameipamba shirki katika nafsi za madhaalimu wapinzani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, yule ambaye alikua amekufa katika upotofu, ameangamia kisha tukaufufua moyo wake kwa Imani, tukamuongoza kwenye Imani na tukamuafikia kuwafuata Mitume Wake, akawa anaishi kwenye miangaza ya uongofu, atakuwa ni kama mfano wa yule aliye ndani ya ujinga, matamanio ya moyo na namna mbalimbali za upotevu, asiyeongokewa kwenye sehemu yoyote ya kupenya na hana wa kumuokoa na yale ambayo yumo ndani yake? Hao wawili hawalingani. Na kama nilivyomuachilia kafiri huyu anayebishana na nyinyi, enyi Waumini, nikampambia vitendo vyake viovu akaviona ni vyema, vilevile nimewapambia wenye kukanusha vitendo vyao viovu ili wapaswe, kwa hilo, kupata adhabu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net