Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 121

Al-An'aam 6:121

الأنعام

وَلَا تَأْكُلُوا۟ مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ ٱسْمُ ٱللَّهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُۥ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ ٱلشَّيَـٰطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰٓ أَوْلِيَآئِهِمْ لِيُجَـٰدِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ

Maana

Wala msile katika vile ambavyo halikutajwa jina la Mwenyezi Mungu juu yake. Kwani huko hakika ni kuvuka mipaka. Na kwa yakini mashetani wanawaletea wahyi marafiki zao ili wabishane nanyi. Na mkiwatii, basi nyinyi kwa hakika mtakuwa washirikina.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu. Kwani huo ni upotofu. Na kwa yakini mashet'ani wanawafunza marafiki zao kubishana nanyi. Na mkiwafuata basi hapana shaka nyinyi mtakuwa washirikina. [121]

[121] Ilivyo kuwa hao wanyama ni halali kwenu kwa kuwachinja, basi msile yule ambaye hakutajiwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kumchinja, ikiwa limeachwa kutajwa makusudi, au limetajwa jina jingine lisilo kuwa la Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani hivyo ni upotovu, na kutokana na hukumu ya Mwenyezi Mungu! Na hakika majeuri, Iblisi na wasaidizi wake, huwatia tia katika vifua vya wale walio kwisha watawala, ili wajadiliane nanyi kwa upotovu, na wakupelekeeni kuharimisha alivyo halalisha Mwenyezi Mungu. Nanyi mkiwafuata mtakuwa mfano wao katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wala msile, enyi Waislamu, katika vichinjwa, yule ambaye halikutajwa jina la Allah Mtukufu wakati wa kuchinjwa, kama mfu na aliochinjiwa masanamu na majini na wasiokuwa hao. Na kwa hakika kuwala wanyama hao ni kutoka kwenye twaa ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka. Na majini waasi wanawatia marafiki zao, miongoni mwa mashetani wa kibinadamu, ushawishi wa kuwatatiza kuhusu uharamu wa kula mfu; wanawaamrisha wawaambie Waislamu wanapobishana nao, «Hakika nyinyi, kwa kutokula kwenu mfu, huwa hamli anachokiua Allah Mtukufu, ambapo mnakula mnachokichinja.» Na iwapo mtawasikiliza, enyi Waislamu, katika kuhalalisha mfu, basi nyinyi mtakuwa sawa na wao katika ushirikina.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net