Al-An'aam 6:120
الأنعاموَذَرُوا۟ ظَـٰهِرَ ٱلْإِثْمِ وَبَاطِنَهُۥٓ ۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكْسِبُونَ ٱلْإِثْمَ سَيُجْزَوْنَ بِمَا كَانُوا۟ يَقْتَرِفُونَ
Na acheni dhambi iliyo dhahiri na iliyofichikana yake. Hakika wale wanaochuma dhambi watalipwa kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na acheni dhambi zilizo dhaahiri na zilizo fichikana. Hakika wanao chuma dhambi watalipwa kwa waliyo kuwa wakiyachuma. [120]
[120] Sio uchamngu kuharimisha alicho halalisha Mwenyezi Mungu. Hakika uchamngu ni kuacha madhambi ya nje na ndani. Basi wacheni madhambi katika vitendo vyenu, vinavyo onekana na vilivyo fichika. Na bila ya shaka wanao chuma madhambi watalipwa kwa kadri ya madhambi wayatendayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na acheni, enyi watu, maasia yote, yaliyo waziwazi na yaliyo ya siri. Hakika wale wanaofanya maasia, Mola wao Atawatesa kwa sababu ya yale maovu ambayo walikuwa wakiyafanya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net