Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 119

Al-An'aam 6:119

الأنعام

وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا۟ مِمَّا ذُكِرَ ٱسْمُ ٱللَّهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا ٱضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا لَّيُضِلُّونَ بِأَهْوَآئِهِم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُعْتَدِينَ

Maana

Na mna nini msile katika vile vilivyotajiwa jina la Mwenyezi Mungu, naye amekwishawabainishia kwa kina vile alivyowaharamishia, isipokuwa vile mnavyolazimishwa? Na hakika wengi wanapotea kwa matamanio yao bila ya kuwa na elimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye kujua vyema wale wanaopindukia mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kwa nini msile katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, naye amekwisha kubainishieni alivyo kuharimishieni, isipo kuwa vile mnavyo lazimishwa? Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio yao bila ya kuwa na ilimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua wanao pindukia mipaka. [119]

[119] Na hakika hapana sababu yoyote au dalili ya kukuzuieni kula nyama aliye tajiwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yake wakati wa kuchinja miongoni mwa nyama hoa. (yaani nyama wa kufuga.) Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika na Aliye tukuka amekwisha kubainishieni vilio harimishwa, katika hali isiyo kuwa ya dharura, kama mzoga na damu (na nguruwe). Watu wengi wanaacha Haki, si kwa lolote, ila kufuata pumbao la nafsi zao tu, bila ya kuwa wamepewa ilimu, au hoja iliyo thibiti kwao. Kama hao Waarabu walio jiharimishia wenyewe baadhi ya wanyama wa kufuga. Wala nyinyi hamna makosa kwa kula kilicho zaliwa, bali wao ndio wamepita mipaka kwa kuharimisha kilicho halali. Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mjuzi wa hao walio pindukia mipaka kwa ujuzi usio na mfano wake kwa hakika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kitu gani kinachowazuia, enyi Waislamu, kumla mnyama ambaye jina la Allah Mtukufu lilitajwa wakati wa kuchinjwa, ambapo Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Amewaelezea nyinyi yote aliyoyaharamisha kwenu? Lakini yale ya haramu ambayo dharura imepelekea yatumiwe, kwa sababu ya njaa, kama mfu, basi mumehalalishiwa. Na wengi, kati ya wapotofu, wanawapoteza wafuasi wao na kuwaepusha na njia ya Allah Mtukufu katika kuhalalisha haramu na kuharamisha halali kwa matakwa yao kwa ujinga walionao. Kwa hakika, Mola wako, ewe Mtume, Ndiye Amjuwaye zaidi yule aliyekiuka mipaka Yake katika hayo; na Yeye Ndiye Atakayesimamia hesabu yake na malipo yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net