Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 118

Al-An'aam 6:118

الأنعام

فَكُلُوا۟ مِمَّا ذُكِرَ ٱسْمُ ٱللَّهِ عَلَيْهِ إِن كُنتُم بِـَٔايَـٰتِهِۦ مُؤْمِنِينَ

Maana

Basi kuleni katika vile vilivyotajiwa jina la Mwenyezi Mungu, ikiwa mnaziamini Aya zake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi kuleni katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, ikiwa mnaziamini Aya zake. [118]

[118] Ilivyo kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye anaye wajua walio hidika na walio potea, basi msielekee kwenye upotovu wa washirikina wa kuharimisha baadhi ya nyama hoa (nyama wa kufuga). Basi kuleni katika hao, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu amekuruzukuni hao, na amewafanya ni halali na wazuri, na hapana madhara kuwala. Na mnapo wachinja litajeni jina la Mwenyezi Mungu juu yao, maadamu nyinyi mnamuamini Yeye na mnamnyenyekea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi kuleni, kati ya wanyama waliochinjwa, wale ambao jina la Allah Mtukufu lilitajwa wakati wa kuchinjwa, iwapo nyinyi mnaziamini hoja za Allah Mtukufu, aliyetukuka, zilizo wazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net