Al-An'aam 6:117
الأنعامإِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ مَن يَضِلُّ عَن سَبِيلِهِۦ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُهْتَدِينَ
Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayejua vyema yule aliyepotea Njia yake, naye ndiye anayejua vyema wale walioongoka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua walio potea Njia yake, na ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua walio hidika. [117]
[117] Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye kujua kwa ujuzi ambao hapana mfano wake, kuwajua hao ambao wamekuwa mbali na Njia ya Haki, na hao ambao wameongoka na uwongofu ukawa ndio sifa yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika, Mola wako Ndiye Anayewajua zaidi wenye kupotea njia ya uongofu; na Yeye anawajua zaidi, kuliko nyinyi, wale walio kwenye njia ya uongofu na usawa; hafichiki Kwake yoyote katika wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net