Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 116

Al-An'aam 6:116

الأنعام

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِى ٱلْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ

Maana

Na ukiwatii wengi wa hawa walio katika dunia, watakupoteza mbali na Njia ya Mwenyezi Mungu. Hawa hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa isipokuwa ni wenye kusema uongo tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ukiwat'ii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Mwenyezi Mungu. Hawa hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu. [116]

[116] Na ikiwa Subhanahu ndiye mwenye hukumu ya uadilifu inayo rejewa kwenye Vitabu vyake katika kutafuta Haki na kuijua, basi ewe Nabii, usiwe wewe na walio pamoja nawe, mkamfuata yeyote anaye achana na kauli ya Haki, hata ikiwa hao ni wengi wa idadi. Kwani ukiwafuata aghlabu ya watu ambao hawategemei Sharia iliyo teremshwa na Mwenyezi Mungu, watakuweka mbali na Njia ya Haki iliyo nyooka. Na hiyo ndiyo Njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na watu hao hawendi ila nyuma ya dhana na mawazo tu, na wala hawasemi ila kwa kukisia tu; hawategemei hoja na ushahidi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau itakadiriwa, ewe Mtume, kwamba wewe uwasikilize wengi kati ya watu wanaokaa ardhini, kwa kweli wangekupoteza ukawa kando na dini ya Allah Mtukufu. Kwani wao hawaendi isipokuwa kwenye yale wanayoyaona kuwa ni haki kwa kuwaiga wakale wao. Na hawakuwa wao isipokuwa tu wanadhania na wanasema urongo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net