Al-An'aam
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِى ٱلْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ 116
{116} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad-rehema na Amani zimshukie – akimtahadharisha juu ya kuwatii wengi wa watu: "Na ukiwatii wengi wa hawa waliomo katika dunia, watakupoteza na Njia ya Mwenyezi Mungu." Kwa maana wengi wao, walikwisha potoka katika dini zao, na matendo yao, na elimu zao. Hivyo basi dini zao ni mbovu, na matendo yao yanafuata matamanio yao, na elimu zao hazina uhakika wala kufikisha katika njia iliyo sawa. Bali ukomo wao ni kwamba wanafuata dhana ambayo haifai kitu mbele ya haki, na wanadanganya katika kusema juu ya Mwenyezi Mungu kwa yale wasiyoyajua.