Al-An'aam 6:115
الأنعاموَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَـٰتِهِۦ ۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ
Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa ukweli na uadilifu. Hakuna yeyote wa kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa kweli na uadilifu. Hapana awezaye kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. [115]
[115] Na hakika hukumu ya Mwenyezi Mungu imekwisha toka. Basi maneno ya Mola wako Mlezi ya kweli na ya uadilifu yametimia kwa kuteremshwa Kitabu hichi Kitukufu, chenye kukusanya ukweli. Na ndani imo mizani ya kweli ya kupimia Haki na upotovu. Wala hapana wa kuyageuza maneno ya Mwenyezi Mungu na Kitabu chake. Naye Subhana ni Mwenye kusikia kila lisemwalo, Mwenye kukijua kila kinacho toka kwao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na limekamilika neno la Mola wako, nalo ni Qur’ani, likiwa lina ukweli wa habari na maneno, lenye uadilifu wa hukumu. Hakuna anayeweza kuyabadilisha maneno yake yaliyokamilika. Na Allah Mtukufu, Ndiye Mwenye kuyasikia wanayoyasema waja Wake, Ndiye mwenye kuyajua mambo yao yaliyo waziwazi na yaliyojificha
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net