Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 114

Al-An'aam 6:114

الأنعام

أَفَغَيْرَ ٱللَّهِ أَبْتَغِى حَكَمًا وَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ إِلَيْكُمُ ٱلْكِتَـٰبَ مُفَصَّلًا ۚ وَٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَـٰهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُۥ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِٱلْحَقِّ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُمْتَرِينَ

Maana

Je, nimtafute hakimu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliyewateremshia Kitabu hiki kilichoelezwa kwa kina? Na wale tuliowapa Kitabu wanajua ya kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa Haki. Basi kamwe usiwe katika wale wanaotia shaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni Kitabu kilicho elezwa waziwazi? Na hao tulio wapa Kitabu wanajua ya kwamba kimeteremshwa na Mola wako Mlezi kwa Haki. Basi usiwe katika wanao tia shaka. [114]

[114] Ewe Nabii! Waambie: Hii ni hukumu ya Mwenyezi Mungu kwa Haki, iliyo bainishwa na Aya zilio zagaa. Basi haijuzu nitafute hukumu isiyo kuwa yake Yeye ya kutupambanua baina yangu na nyinyi. Mwenyewe Subhana kesha hukumu, na ameteremsha Kitabu kitukufu kiwe ni hoja juu yenu. Nanyi mmeshindwa kuleta mfano wake. Nacho kinabainisha Haki na uadilifu. Na wale walio pewa Kitabu wanajua kuwa hii Qur'ani imetoka kwa Mwenyezi Mungu, na imekusanya Haki, kama vilivyo bashiri vitabu vyao, ijapo kuwa wanajaribu kuyaficha hayo. Basi wewe Nabii, pamoja na walio kufuata, msiwe katika wenye kutilia shaka Haki baada ya kubainishwa kwake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Kwani kwa asiyekuwa Allah Mtukufu, Aliye Mola wangu na Mola wenu, natafuta uamuzi kati yangu na nyinyi, na hali Yeye, kutakasika na sifa pungufu ni Kwake, Amewateremshia Qur’ani ambayo ndani yake pana ufafanuzi wa uamuzi wa yale ambayo mlikuwa mkiteta juu yake kuhusu mambo yangu na mambo yenu?» Na Wana wa Isrãîl waliopewa na Allah Mtukufu Taurati na Injili wana ujuzi wa yakini kwamba hii Qur’ani imeteremshwa kwako, ewe Mtume, kutoka kwa Mola wako kwa haki. Basi usiwe, tena usiwe ni miongoni mwa wenye shaka juu ya chochote ambacho tumekuletea wahyi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net