Al-An'aam 6:113
الأنعاموَلِتَصْغَىٰٓ إِلَيْهِ أَفْـِٔدَةُ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ وَلِيَرْضَوْهُ وَلِيَقْتَرِفُوا۟ مَا هُم مُّقْتَرِفُونَ
Na ili ziyaelekee hayo nyoyo za wale wasioiamini Akhera, nao wayaridhie, na wayachume yale wanayoyachuma.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ili nyoyo za wasio amini Akhera zielekee hayo, nao wayaridhie na wayachume wanayo yachuma. [113]
[113] Wao huyapindua maneno ya upotovu wazidanganye nafsi zao na ziridhie, na zielekee huko huko vile vile nyoyo za walio kama wao majeuri wasio iogopa Akhera, wanao itakidi kuwa uhai ni dunia tu, na waingie katika madhambi na maasi kwa sababu ya kuto iamini kwao Siku ya Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ili zielekee huko nyoyo za makafiri ambao hawaamini maisha ya Akhera wala hawayafanyii matendo ya kuwafaa, na ili nafsi zao zipate kuyapenda, na ili wapate kuyafanya maovu ambayo wao ni wenye kuyafanya. Katika haya, pana onyo kubwa kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net