Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 112

Al-An'aam 6:112

الأنعام

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِىٍّ عَدُوًّا شَيَـٰطِينَ ٱلْإِنسِ وَٱلْجِنِّ يُوحِى بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ ٱلْقَوْلِ غُرُورًا ۚ وَلَوْ شَآءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ

Maana

Na kadhalika tumemfanyia kila Nabii maadui mashetani wa kiwatu, na kijini, wanafundishana wao kwa wao maneno ya kupambapamba, kwa udanganyifu. Na angelipenda Mola wako Mlezi, wasingelifanya hayo. Basi waache na hayo wanayoyazua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kadhaalika tumemfanyia kila Nabii maadui mashet'ani wa kiwatu, na kijini, wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupamba-pamba, kwa udanganyifu. Na angeli penda Mola wako Mlezi wasingeli fanya hayo. Basi waache na wanayo yazua. [112]

[112] Kama ilivyo kuwa hao wamekufanyia uadui na inadi, na hali wewe unataka kuwaongoa, basi kadhaalika tumemfanyia kila Nabii anaye peleka ujumbe wetu, maadui katika wanaadamu majeuri na majini majeuri, ambao wanajificha kwako na huwaoni, wakitiliana wasiwasi kwa maneno ya kupamba-pamba na udanganyifu, yasiyo na ukweli. Basi kwa hayo huingiza ghururi kwa uwongo! Na hayo yote ni kwa kudra ya Mwenyezi Mungu na kutaka kwake. Na lau angeli taka wasingeli fanya hayo. Lakini hayo ni kwa ajili ya kuzisafisha nyoyo za Waumini. Basi waachilie mbali hao walio potea na kufuru zao za maneno yao wanayo yazua.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kama tulivyokujaribu wewe, ewe Mtume, kwa maadui zako miongoni mwa washirikina, tuliwajaribu Manabii wote, amani iwashukie, kwa maadui miongoni mwa waasi wa watu wao na maadui miongoni mwa waasi wa majini, wanapelekeana wenyewe kwa wenyewe maneno waliyoyapamba kwa uharibifu, ili adanganyike mwenye kuyasikia na apate kupotea njia ya Allah Mtukufu. Na lau Mola wako, Aliyetukuka na kuwa juu, angetaka, angaliweka kizuizi kati yao na ule uadui, lakini huo ni mtihani kutoka kwa Allah Mtukufu. Basi waache na kile wanachokibuni cha urongo na uzushi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net