Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
Sura ya 6

Al-An'aam

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 112

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِىٍّ عَدُوًّا شَيَـٰطِينَ ٱلْإِنسِ وَٱلْجِنِّ يُوحِى بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ ٱلْقَوْلِ غُرُورًا ۚ وَلَوْ شَآءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ 112

{112} Yeye Mtukufu anasema, akimfariji Mtume Wake [Muhammad] - Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani. - Na kama vile tulivyokufanyia maadui wanaoukataa wito wako, na wanakupiga vita, na wanakuhusudu, basi hii ndiyo sunnah yetu, kwamba tunamfanyia maadui kila Nabii tunayemtuma kwa viumbe, miongoni mwa mashetani wa watu, na majini, wanaopinga yale waliyoyaleta Mitume. "Wanafundishana wao kwa wao maneno ya kupambapamba, kwa udanganyifu." Yaani, baadhi yao wanawapambia wenzi wao jambo ambalo wanalingania la batili, na wanalipambia misemo mpaka walifanye katika umbo nzuri zaidi ili wapumbavu wadanganywe nalo, na walifuate wajinga ambao hawafahamu uhakika wala hawaelewi maana zake. Bali wanavutiwa tu na maneno yaliyopambwa, na misemo iliyofichwa, kwa hivyo wanaitakidi haki kwamba ni batili, na batili kwamba ni haki.