Al-An'aam 6:111
الأنعاموَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَآ إِلَيْهِمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ ٱلْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَىْءٍ قُبُلًا مَّا كَانُوا۟ لِيُؤْمِنُوٓا۟ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ
Na lau kuwa tungeliwateremshia Malaika, na maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado hawakuwa ni wa kuamini, isipokuwa Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao hawajui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
NA LAU kuwa tungeli wateremshia Malaika, na maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado wasingeli amini, ila Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao wamo ujingani. [111]
[111] Hakika hao walio apa kuwa ikiwajia Ishara wataiamini, ni waongo. Mwenyezi Mungu anaijua vilivyo imani yao. Lau kuwa sisi tungeli teremsha Malaika wakawaona kwa macho, na maiti wakawasemeza baada ya kufufuliwa makaburini mwao, na kuwakusanyia kila kitu mbele yao kikiwakabili na kuwabainishia haki, bado wasingeli amini ila akipenda Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa waamini. Na wengi hawaitambui Haki wala hawaifuati, kwa sababu nyoyo zao zimesibiwa na upofu wa kijahiliya.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau kama sisi tungaliyaitikia maombi ya washirikina hawa na kuwateremshia Malaika kutoka mbinguni na tukawafufulia wafu wakazungumza nao na tukawakusanyia kila kitu walichokitaka wakakiona ana kwa ana, hawangaliyakubali yale uliyowaitia, ewe Mtume, na hawangaliyatumia, isipokuwa yule ambaye Allah Mtukufu Alimtakia uongofu. Lakini wengi wa hawa makafiri hawaijui haki ambayo umekuja nayo kutoka kwa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net