Ad-Dukhaan 44:4
الدخانفِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ
Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima! [4]
[4] Katika usiku huu wenye baraka hupambanuliwa baina ya mambo yote yenye hikima, na Qur'ani ndio kilele cha hikima, na ndio pambanuo baina ya kweli na uwongo. Na kwa hivyo ndio ikateremshwa katika usiku huo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Katika usiku huo linaamuliwa na kupambanuliwa, kutoka kwenye Ubao Uliohifadhiwa na kuletewa waandishi kati ya Malaika, kila jambo lililokadiriwa la muda wa kuishi na riziki katika mwaka huo, na mambo mengine yatakayokuwa, na kukadiriwa na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, mpaka mwisho wa mwaka, hayabadilishwi wala hayageuzwi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net