Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 44 · Aya ya 3

Ad-Dukhaan 44:3

الدخان

إِنَّآ أَنزَلْنَـٰهُ فِى لَيْلَةٍ مُّبَـٰرَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ

Maana

Hakika Sisi tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji. [3]

[3] Hakika Sisi tumeanza kuiteremsha Qur'ani katika usiku ulio jaa kheri, wenye baraka nyingi, kwani ni mwendo wetu kuonya kwa kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tuliiteremsha katika Usiku wa Cheo uliobarikiwa wenye kheri nyingi, nao unapatikana katika mwezi wa Ramadhani. Sisi ni wenye kuonya watu kwa kile kinachowanufaisha na kuwadhuru, nako ni kule kupeleka Mitume na kuteremsha Vitabu, ili hoja ya Allah Mtukufu iwasimamie waja Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ad-Dukhaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net