Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 44 · Aya ya 5

Ad-Dukhaan 44:5

الدخان

أَمْرًا مِّنْ عِندِنَآ ۚ إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ

Maana

Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma. [5]

[5] Nakusudia kwa jambo hili, yaani jambo kuu lenye kutoka kwetu kama ilivyo kwisha pita hukumu ya mpango wetu. Kwani ni shani yetu kutuma Mitume kwa Vitabu ili kuwafikishia waja wetu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mambo haya yaliyopangwa kimadhubuti ni amri inayotoka kwetu, kwani yote yanayokuwa na Anayokadiria Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na wahyi Anaouleta, vyote hivyo vinatokana na amri Yake na idhini Yake na ujuzi Wake. Hakika sisi tumetuma Mitume, Muhammad na waliokuwa kabla yake, kwa watu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ad-Dukhaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net