Ad-Dukhaan 44:6
الدخانرَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ
Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. [6]
[6] Kwa ajili ya rehema ya Mola wako Mlezi kwa waja wake, amewatuma Mitume kwa watu wawafikishie uwongofu wake, kwani hakika Yeye peke yake, ndiye Mwenye kusikia kila cha kusikiwa, Mwenye kujua kila cha kujuulikana.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hilo likiwa ni rehema kutoka kwa Mola wako, ewe Mtume, kuwafikia wale wenye kutumiwa. Hakika Yeye ni Msikizi, Anasikia sauti zote, ni Mjuzi wa mambo yote ya waja Wake yaliyojitokeza nje na yanayofichika.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net