Ad-Dukhaan 44:7
الدخانرَبِّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَآ ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini. [7]
[7] Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini na haki, na mnaifuata, na mnaamini kuwa hakika ndio Yeye Mwenye kuteremsha Qur'ani kuwa ni rehema na uwongofu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Muumba mbingu na ardhi na vitu vyote vilivyoko baina ya hivyo viwili. Iwapo nyinyi mna yakini na hilo, basi jueni kuwa Mola wa viumbe Ndiye Mola wa kweli,
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net