Al-Ankaboot 29:65
العنكبوتفَإِذَا رَكِبُوا۟ فِى ٱلْفُلْكِ دَعَوُا۟ ٱللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ فَلَمَّا نَجَّىٰهُمْ إِلَى ٱلْبَرِّ إِذَا هُمْ يُشْرِكُونَ
Na wanapopanda katika marikebu, humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumkusudia yeye tu dini yake. Lakini anapowavua wakafika nchi kavu, mara wanamshirikisha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanapo panda katika marikebu, humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafia ut'iifu. Lakini anapo wavua wakafika nchi kavu, mara wanamshirikisha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanapopanda makafiri kwenye majahazi baharini, na wakaogopa kuzama, wanampwekesha Allah Mtukufu na kumtakasia dua wakati wa shida yao. Na Anapowaokoa akawafikisha kwenye nchi kavu, na shida ikawaondokea, wanarudi kwenye ushirikina wao. Hakika yao wao, kwa kufanya hivi, wanagongana, wanampwekesha Allah Mtukufu kipindi cha shida na wanamshirikisha kipindi cha raha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net