Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 64

Al-Ankaboot 29:64

العنكبوت

وَمَا هَـٰذِهِ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَآ إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ ۚ وَإِنَّ ٱلدَّارَ ٱلْـَٔاخِرَةَ لَهِىَ ٱلْحَيَوَانُ ۚ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ

Maana

Na haya maisha ya dunia si chochote isipokuwa ni pumbao na mchezo. Na hakika nyumba ya Akhera ndiyo maisha hasa; laiti wangelikuwa wanajua!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na nyumba ya Akhera ndiyo maisha khasa; laiti wangeli kuwa wanajua!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na haukuwa uhai huu wa ulimwengu isipokuwa ni pumbao na mchezo wa kuzifanya nyoyo zipumbae na miili icheze, kwa sababu ya pambo na matamanio, kisha yanaondoka haraka. Na kwa hakika, nyumba ya Akhera ndiyo uhai wa kikweli na wa daima usiokuwa na kifo ndani yake. Lau watu wangelijua hilo wasingefadhilisha nyumba ya kutoweka juu ya Nyumba ya kusalia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net