Al-Ankaboot
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَمَا هَـٰذِهِ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَآ إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ ۚ وَإِنَّ ٱلدَّارَ ٱلْـَٔاخِرَةَ لَهِىَ ٱلْحَيَوَانُ ۚ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ 64
{64} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya hali ya dunia na Akhera, kwa njia ambayo ndani yake kuna kukatisha tamaa na juu ya dunia hii, na kutia moyo juu ya akhera. Alisema, "Na haya maisha ya dunia" kwa uhakika "si chochote isipokuwa ni pumbao na mchezo" mioyo huyafurahia na miili inayachezea, kwa sababu ya kile ambacho Mwenyezi Mungu aliweka ndani yake cha mapambo, ladha, na matamanio ambayo yanaoneka kwamba ni mazuri kwa mioyo iliyopeana mgongo, ambayo ni marembo kwa macho yaliyoghafilika, yenye kufurahisha roho za wana batili, kisha yanaondoka haraka na kuisha kabisa, mwenye kuyapenda akawa hajapata kwayo isipokuwa majuto, huzuni, na hasara. Ama nyumba ya Akhera, hiyo ndiyo nyumba ya "maisha hasa," ambayo inalazimu kwamba miili ya watu wake ni yenye nguvu sana, ambayo imeumbwa kwa ajili ya uzima, na kwamba ina kila kitu ambacho kinaufanya uhai kuwa kamili, na raha yake inakuwa kamilifu kwa mambo yanayofurahisha mioyo na ya yale yanayotamaniwa na miili kama vile vyakula, vinywaji, ndoa, na mengineyo miongoni mwa mambo ambayo jicho halijawahi kuona, wala hakuna sikio lililowahi kusikia, wala hayajawahi kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote. "Laiti wangelikuwa wanajua," basi wasingelipendelea dunia kuliko Akhera. Na kama wangelikuwa wanatumia akili, basi wasingelipenda nyumba ya pumbao na mchezo na wakaacha nyumba ya uhai halisi. Kwa hivyo, hilo likaashiria kwamba wale wanaojua ni lazima waipenedlee Akhera kuliko dunia, kwa sababu wanajua hali halisi za nyumba mbili hizi.