Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Ankaboot
Sura ya 29

Al-Ankaboot

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya 65–66

فَإِذَا رَكِبُوا۟ فِى ٱلْفُلْكِ دَعَوُا۟ ٱللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ فَلَمَّا نَجَّىٰهُمْ إِلَى ٱلْبَرِّ إِذَا هُمْ يُشْرِكُونَ 65 لِيَكْفُرُوا۟ بِمَآ ءَاتَيْنَـٰهُمْ وَلِيَتَمَتَّعُوا۟ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ 66

{65 - 66} Kisha Mwenyezi Mungu aliwafanya washirikina kukubali suala kwamba kwa kuwa wanamkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika ugumu, wanapokuwa wanasafiri baharini na mawimbi yake yakawa makali na wakaogopa kuangamia; hapo wao huwaacha masanamu wao, na wanamkusudia kwa dua yao Mwenyezi Mungu tu asiyekuwa na mshirika. Na pindi ugumu huo unapoisha na akawaokoa hadi nchi kavu Yule ambaye walimkusudia katika dua yao, wakamshirikisha na yule ambaye hakuwaokoa katika ugumu huo, wala hakuwaondolea shida yao. Basi kwa nini hawamkusudii Mwenyezi Mungu kwenye dua zao katika hali ya furaha na shida, na wepesi na ugumu, ili wamuamini kiuhakika, na wastahiki thawabu zake, na wazuilike kutokana na adhabu yake. Lakini wao wanafanya ushirikina baada ya sisi kuwaneemesha na kuwaokoa kutoka baharini ili uwe mwisho wake wake ni kukufuru yale tuliyowapa, na kufanya ubaya baada ya kuneemeshwa, na ili wakamilishe starehe zao katika dunia, ambayo ni kama starehe wanazofanya wanyama, wakawa hao hawana hamu yoyote isipokuwa tumbo zao na tupu zao. "Lakini watakuja jua" watakapoondoka duniani kwenda Akhera, ukubwa wa majuto yao na adhabu chungu.