Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Ankaboot
Sura ya 29

Al-Ankaboot

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 67

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّا جَعَلْنَا حَرَمًا ءَامِنًا وَيُتَخَطَّفُ ٱلنَّاسُ مِنْ حَوْلِهِمْ ۚ أَفَبِٱلْبَـٰطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَةِ ٱللَّهِ يَكْفُرُونَ 67

{67} Kisha akawakumbusha neema yake juu yao kwa kuwapa mahali patakatifu penye amani, na kwamba wao ndio wenye hapo na wanaishi kwa amani na wasaa na riziki nyingi, ilhali watu waliowazunguka wanatekwa nyara na wana hofu. Basi kwa nini hawamwabudu yule ambaye aliwalisha wasipate njaa, na akawalinda kutokana na hofu? "Je, wanaamini batili," ambayo ni huo ushirikina wao na maneno na matendo batili, "na neema za Mwenyezi Mungu wanazikufuru?" Akili zao zilienda wapi, na ni wapi maono yao yalipotelea, kwa maana walipendelea upotofu badala ya uwongofu, na batili badala ya haki, na mashaka badala ya furaha, na ambapo walikuwa wao ndio madhalimu zaidi ya viumbe wote?