Al-Ankaboot 29:66
العنكبوتلِيَكْفُرُوا۟ بِمَآ ءَاتَيْنَـٰهُمْ وَلِيَتَمَتَّعُوا۟ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
Wapate kuyakufuru yale tuliyowapa, na wajistareheshe. Lakini watakuja jua!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wapate kuyakanya tuliyo wapa, na wajistareheshe. Lakini watakuja jua!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kushirikisha kwao baada ya sisi kuwaneemesha kwa kuwaokoa na bahari, ni ili iwe mwisho wake ni kuzikanusha zile tulizowaneemesha katika nafsi zao na mali zao na ili wakamilishe kujistarehesha kwao katika hii dunia. Basi wataujua uharibikaji wa matendo yao na kile Alichowaandalia wao Allah Mtukufu cha adhabu kali Siku ya Kiyama. Na katika hilo pana onyo na tahadharisho kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net