Al-Baqara 2:254
البقرةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَنفِقُوا۟ مِمَّا رَزَقْنَـٰكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِىَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَـٰعَةٌ ۗ وَٱلْكَـٰفِرُونَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ
Enyi mlioamini! Toeni katika tulivyowaruzuku kabla haijakuja Siku ambayo hapatakuwapo biashara yoyote, wala urafiki, wala uombezi. Na makafiri ndio madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Toeni katika tulivyo kupeni kabla haijafika Siku ambayo hapatakuwapo biashara, wala urafiki, wala uombezi. Na makafiri ndio madhaalimu. [254]
[254] Enyi mlio muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho! Toeni baadhi ya tuliyo kuruzukuni kwa ajili ya mambo ya kheri. Fanyeni haraka kwa hayo kabla haijafika Siku ya Kiyama ambayo itayo kuwa yote ni ya kheri, wala hazipatikani sababu za kuzozana. Siku hiyo hamwezi kuyadiriki yaliyo kwisha kupiteni duniani, na hapo haitakufaeni biashara, wala urafiki, wala uombezi wa mtu yeyote bila ya idhini ya Mwenyezi Mungu. Na siku hiyo dhulma za makafiri zitadhihiri kwa kuwa hawakuitikia Wito wa Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na kumsadiki Mtume Wake na kufanya amali zinazoambatana na uongofu Wake! Toeni Zaka zilizofaradhiwa na mtoe sadaka ya vitu mlivyopewa na Allah Mtukufu kabla haijaja Siku ya Kiyama, wakati ambapo hakuna kuuziana ikapatikana faida, wala mali ambayo nyinyi mtajikomboa nayo nafsi zenu kutokana na adhabu ya Allah Mtukufu, wala urafiki wa rafiki wenye kuwaokoa, wala muombezi anayemiliki kuwafanya mpunguziwe adhabu. Na makafiri ndio madhalimu na wakeukaji mipaka ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net