Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 72

An-Nahl 16:72

النحل

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَٰجًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنْ أَزْوَٰجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةً وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ ۚ أَفَبِٱلْبَـٰطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَتِ ٱللَّهِ هُمْ يَكْفُرُونَ

Maana

Na Mwenyezi Mungu amewaumbia wake kutokana na nyinyi wenyewe, na akawafanyia kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akawaruzuku vitu vizuri. Basi je, wanaamini upotovu na wanazikufuru neema za Mwenyezi Mungu?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akakuruzukuni vitu vizuri vizuri.Basi je, wanaamini upotovu na wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu? [72]

[72] Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake wa jinsi yenu mtulie nao. Tena amekupeni, kutoka kwa wake zenu, wana na wajukuu, na akakuruzukuni vitu vya kufurahisha nafsi zenu alivyo kuhalalishieni. Je, baada ya haya ndio baadhi ya watu humshirikisha Mwenyezi Mungu, na wakaamini upotovu, na wakazipinga neema za Mwenyezi Mungu zinazo onekana, ambazo zinastahiki shukrani kutoka kwao, na kumsafia ibada Mwenyezi Mungu? Ndoa ni mfungamano mtakatifu ambao ndio asili ya ukoo na kiini cha umma na jamii. Na ndoa ni mpango wa kuidhibiti ile khulka waliyo nayo wanaadamu na wanyama, nayo ni kutamani kuingiliana. Lau ingeli kuwa hapana ndoa iliyo kadiriwa kudhibiti ile khulka ya kutamaniana basi binaadamu wangeli kuwa sawa na wanyama kwa kufuata fujo na uchafu wa kuingiliana. Na hapo mwanaadamu asingeli kuwa yule kiumbe aliye mjaalia Mwenyezi Mungu kuwa na akili na fikra na akamtukuza kuliko viumbe vyengine, na akamrithisha mamlaka ya ardhi. Ilivyo kuwa mpango wa Mwenyezi Mungu katika uhai huu ni kutengeneza khulka kwa ndoa ili binaadamu awe juu kuliko wanyama wengine, hali kadhaalika binaadamu kwa upande mwengine ameumbiwa kupenda kubakia. Na ilivyo kuwa hapana njia ya kubakia yeye mwenyewe, naye anayajua hayo kutokana na baba zake na babu zake na vitu vyote vilio hai, basi njia pekee ni yeye kuzaa dhuriya wapate kuishi na kuendelea daima. Na labda lenye kuweka wazi kabisa ile khulka yake ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akakuruzukuni vitu vizri vizuri."

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Amewaumba wake kutokana na na nyinyi ili nafsi zenu ziliwazike na wao, na amewapa kutokana nao watoto, na kutokana na kizazi chao wajukuu, na Amewaruzuku vyakula vizuri miongoni mwa matunda, nafaka, nyama na visivyokuwa hivyo. Je, kwani wanauamini upotofu wa uungu wa washirika wao na wanazikanusha neema za Allah Mtukufu zisizohesabika na hawamshukuru kwa kumpwekesha Yeye Peke Yake, Aliyetukuka na kuwa juu, kwa ibada?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net