An-Nahl 16:73
النحلوَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَهُمْ رِزْقًا مِّنَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ شَيْـًٔا وَلَا يَسْتَطِيعُونَ
Na badala ya Mwenyezi Mungu wanawaabudu wasiowamilikia riziki kutoka mbinguni wala kwenye ardhi, wala hawawezi kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na badala ya Mwenyezi Mungu wanawaabudu wasio wamilikia riziki kutoka mbinguni wala kwenye ardhi, wala hawawezi kitu. [73]
[73] Na wakawa badala ya Mwenyezi Mungu wakaabudu masanamu ambayo hayawezi kuwapa riziki yoyote hata chembe, sawa sawa ikiwa riziki hiyo inatoka mbinguni kama maji, au kutokana na ardhi kama matunda ya miti na mimea. Na miungu hiyo haiwezi kufanya lolote kama hayo, wala duni ya hayo!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na washirikina wanaabudu masanamu ambayo hayana mamlaka ya kuwapa riziki itokayo mbinguni kama mvua wala itokayo ardhini kama mazao. Wao hawamiliki kitu chochote wala hapana uwezekano wowote kwa wao kukimiliki, kwani wao hawawezi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net