Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 74

An-Nahl 16:74

النحل

فَلَا تَضْرِبُوا۟ لِلَّهِ ٱلْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

Maana

Basi msimpigie Mwenyezi Mungu mifano. Hakika Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi msimpigie Mwenyezi Mungu mifano. Hakika Mwenyezi Mungu anajua,na nyinyi hamjui. [74]

[74] Na ilivyo kuthibitikieni kuwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu hakufaeni kitu, basi msiseme kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ana yeyote wa kumshabihi, ikawa kisingizio cha kuwaabudu hao kwa vipimo vipotovu, na kushabihisha kusio kweli kwa ajili ya kuwaabudu hao pamoja naye! Hakika Mwenyezi Mungu anajua upotovu wa mnayo yatenda, naye atakulipeni kwayo na hali nyinyi mmo katika mghafala hamjui ubaya wa mwisho wenu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mjuapo kwamba masanamu na mizimu havinufaishi, basi msimfanye Allah Mtukufu ana mfano miongoni mwa viumbe Wake mkawa mnawashirikisha wao pamoja na Yeye katika ibada. Hakika Allah Mtukufu Anayajua mnayoyafanya, na nyinyi mumeghafilika hamjui makosa yenu na ubaya wa mwisho wenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net