An-Nahl 16:75
النحلضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَىْءٍ وَمَن رَّزَقْنَـٰهُ مِنَّا رِزْقًا حَسَنًا فَهُوَ يُنفِقُ مِنْهُ سِرًّا وَجَهْرًا ۖ هَلْ يَسْتَوُۥنَ ۚ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtumwa aliyemilikiwa, asiyeweza kitu, na mwingine tuliyemruzuku riziki njema inayotoka kwetu, naye akawa anatoa katika riziki hiyo kwa siri na dhahiri. Je, hao watakuwa sawa? Alhamdu Lillahi (sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu)! Lakini wengi wao hawajui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa mtumwa aliye milikiwa, asiyeweza kitu, na mwingine tuliye mruzuku riziki njema inayo toka kwetu,naye akawa anatoa katika riziki hiyo kwa siri na dhaahiri. Je, hao watakuwa sawa? Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu.Lakini wengi wao hawajui. [75]
[75] * Mwenyezi Mungu amepiga mfano kufahamisha ufisadi walio nao washirikina. Mtumwa aliye milikiwa kama mtumwa mamluki, hanalo aliwezalo kulitenda; na muungwana anaye ruzukiwa na Mwenyezi Mungu riziki ya halali, naye anatoa katika hiyo riziki kwa siri na dhaahiri! Je, ni sawa watumwa wasio weza kitu, na waungwana wenye nacho na wanatumia walicho nacho? Hakika Mwenyezi Mungu anamiliki kila kitu, na anafanya katika ufalme wake kama apendavyo. Na asiye kuwa Yeye hamiliki chochote. Basi huyo hastahiki kuabudiwa na kuhimidiwa. Sifa zote ni haki ya Mwenyezi Mungu peke yake. Yeye ndiye Mwenye Utukufu peke yake, kwani kila kheri inatoka kwake, na kila zuri linarejea kwake. Wala hawatendi hao wanayo yatenda kwa kujua, bali wanatenda kwa kuwafuata wakubwa zao. Bali wengi wao hawajui, na wanaziambatisha neema za Mwenyezi Mungu kwa wengineo, na wanawaabudu hao badala yake!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Amepiga mfano, Akafafanua kwa mfano huo ubatilifu wa itikadi ya washirikina. Mfano wenyewe ni wa mtu aliyemilikiwa asiyeweza kujipitishia jambo asiyemiliki chochote, na mtu mwingine aliye huru, mwenye mali ya halali ambayo Allah Mtukufu Amemruzuku, anayemiliki kupitisha atakalo katika mali hiyo, akawa anapeana kwa siri na kwa dhahiri. Je, kuna yoyote mwenye akili atakayesema kwamba watu wawili hawa wako sawa? Hivyo ndivyo Alivyo Allah Mtukufu Anayemiliki na Anayepitisha. Yeye Hafanani na viumbe Vyake na watumwa wake. Basi vipi mtafananisha baina yao? Sifa njema zote ni za Allah Mtukufu, Peke Yake. Yeye Ndiye Anayestahiki kushukuriwa na kusifiwa. Lakini wengi wa washirikina hawajui kwamba sifa njema na neema ni za Allah Mtukufu na kwamba Yeye, Peke Yake, Ndiye Anayestahiki kuabudiwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net