An-Nahl 16:76
النحلوَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَآ أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَىْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَىٰهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ ۖ هَلْ يَسْتَوِى هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِٱلْعَدْلِ ۙ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa wanaume wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote, naye ni mzigo kwa mlezi wake. Popote anapomuelekeza, haleti heri yoyote. Je, huyo anaweza kuwa sawa na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko kwenye njia iliyonyooka?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa watu wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote, naye ni mzigo kwa bwana wake. Popote anapo muelekeza haleti kheri. Je! Huyo anaweza kuwa sawa na yule anaye amrisha uadilifu,naye yuko juu ya Njia Iliyo Nyooka. [76]
[76] Mwenyezi Mungu amekupigieni mfano mwengine, wa watu wawili. Mmoja wao kiziwi-bubu; hafahamu wala hafahamiki, mzigo kwa aliye mlazimu kumtazama. Bwana wake akimuelekeza kokote harejei na faida yoyote. Basi, je, mtu huyu atakuwa sawa na mtu mwenginewe aliye fasihi wa kusema, anasikia vyema, anaamrisha haki na uadilifu, naye mwenyewe ameshika Njia iliyo kaa sawa, isiyo kwenda upogo? Huyo kiziwi asiye sikia wala kusema wala hafahamu wala hafahamiki, ndio mfano wa masanamu wanayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Kwani hayo hayasikii wala hayasemi wala hayafai kitu. Hayawezi hayo kulingana na Mwenye kusikia, Mwenye kujua, Mwenye kuwaita watu wende kwenye kheri na haki, na kwenye Njia Iliyo Nyooka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Amepiga mfano mwingine wa ubatilifu wa ushirikina. Mfano wenyewe ni wa watu wawili, mmoja wao ni bubu kiziwi, haelewi wala haelezi, hawezi kujinufaisha yeye mwenyewe wala wengine, naye ni mzigo mzito kwa anayesimamia mambo yake na kumwangalia kwa mahitaji yake, akimtuma kwa jambo lolote alitekeleze hafaulu wala hamletei jambo lolote zuri. Na mtu mwengine ana hisia zilizo sawa, anajinufaisha yeye na wengine, anaamuru utunzaji wa haki, na yeye yuko kwenye njia iliyo wazi isiyopotoka. Je, watu wawili hawa wanalingana katika maoni ya wenye akili? Basi vipi mtafananisha baina ya sanamu kiziwi na Allah Mtukufu Muweza Mwenye kuneemesha kila zuri?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net