Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 77

An-Nahl 16:77

النحل

وَلِلَّهِ غَيْبُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَمَآ أَمْرُ ٱلسَّاعَةِ إِلَّا كَلَمْحِ ٱلْبَصَرِ أَوْ هُوَ أَقْرَبُ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Maana

Na siri zote za mbinguni na ardhini ni za Mwenyezi Mungu. Wala halikuwa jambo la Saa (ya Kiyama) isipokuwa kama kupepesa kwa jicho, au chini zaidi ya hivyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na siri zote za katika mbingu na ardhi ziko kwa Mwenyezi Mungu.Wala halikuwa jambo la Saa (ya Kiyama) ila kama kupepesa kwa jicho, au akali ya hivyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. [77]

[77] Na ni ya Mwenyezi Mungu tu peke yake yote wasiyo yajua waja katika mbingu na katika ardhi. Wala jambo la kuja Siku ya Kiyama, na kufufuliwa watu, haraka yake na upesi wake kwa Mwenyezi Mungu, si chochote ila ni kama kufumba na kufumbua jicho! Bali ni duni kuliko hivyo, jinsi ya upesi wake. Hakika uwezo wa Mwenyezi Mungu ni mkubwa mno, Yeye haemewi na kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ni wa Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, ujuzi wa mambo yasiyoonekana ya mbinguni na ardhini. Na jambo la Kiyama haliwi, kwa uharaka wa kuja kwake, isipokuwa ni kama mtazamo wa haraka wa jicho au ni haraka zaidi kuliko huo. Hakika Allah Mtukufu kwa kila jambo ni Muweza.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net