An-Nahl 16:78
النحلوَٱللَّهُ أَخْرَجَكُم مِّنۢ بُطُونِ أُمَّهَـٰتِكُمْ لَا تَعْلَمُونَ شَيْـًٔا وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمْعَ وَٱلْأَبْصَـٰرَ وَٱلْأَفْـِٔدَةَ ۙ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Na Mwenyezi Mungu aliwatoa matumboni mwa mama zenu hali ya kuwa hamjui kitu, na akawajaalia kusikia na kuona na ufahamu wa nyoyo ili mpate kushukuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu amekutoeni matumboni mwa mama zenu, hali ya kuwa hamjui kitu, na amekujaalieni masikio na macho na nyoyo ili mpate kushukuru. [78]
[78] Na Mwenyezi Mungu amekutoeni kutokana na matumbo ya mama zenu hali hamjui chochote katika yaliyo kuzungukeni. Na akakupeni kusikia na kuona na nyoyo, kuwa ndio silaha za kujifunzia na kufahamu, ili mpate kumuamini kwa njia ya ilimu, na mumshukuru kwa alivyo kufadhilini. Utabibu wa kisasa umethibitisha kuwa kuweza kusikia kunaanza mapema sana katika maisha ya mtoto mchanga, mnamo wiki chache za mwanzo. Ama kuona huanza mwezi wa tatu. Wala kuona hakuwi baraabara mpaka katika mwezi wa sita. Ama "moyo " wa kufahamu na kutambua huwa baada ya hayo. Mpango ulio letwa na Qur'ani ni mpango unao lingana na hisiya hizo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Amewatoa nyinyi kutoka kwenye matumbo ya mama zenu baada ya kipindi cha mimba, hali hamtambui chochote kilichoko pambezoni mwenu, na akawapatia sababu za kutambua miongoni mwa masikio ya kusikia na macho ya kuonea na nyoyo, ili mpate kumshukuru Allah Mtukufu Aliyetukuka kwa neema hizo na mkampwekesha, Aliyeshinda na kutukuka, kwa ibada.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net