An-Nahl 16:79
النحلأَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَى ٱلطَّيْرِ مُسَخَّرَٰتٍ فِى جَوِّ ٱلسَّمَآءِ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا ٱللَّهُ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ
Je, hawawaoni ndege walivyotiishwa katika anga la mbingu? Hakuna mwenye kuwashikilia isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hakika katika haya zipo ishara kwa kaumu wanaoamini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Hawawaoni ndege walivyo wat'iifu katika anga la mbingu? Hapana mwenye kuwashika isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Hakika katika haya zipo ishara kwa watu wanao amini. [79]
[79] Je! Hao washirikina hawawaangalii ndege walio jaaliwa waweze kuruka hewani juu, kwa kupewa na Mwenyezi Mungu mbawa kubwa kuliko miili yao, wakiikunjua na kuikunja. Na Mwenyezi Mungu akaidhalilisha hewa kuwabeba hao ndege. Hapana anaye washika huko angani ila Mwenyezi Mungu kwa nidhamu aliyo itengeneza Yeye Mwenyewe! Hakika katika kuwatazama hao ndege, na kuzingatia hikima ya Mwenyezi Mungu katika kuwaumba, ni ishara kubwa ya kuwanafiisha walio kuwa tayari kuamini. Ndege wanaruka kwa sababu kadhaa wa kadhaa katika kuumbwa kwao. Muhimu kuliko yote ni lile umbo lao la kuchongoka, na kuwa mbawa zao zilivyo tanda zenye manyoya, na mafupa yenye uwazi na myepesi na vifuko vya hewa kati ya matumbo yao, navyo vimeambatishwa na mayavuyavu (mapafu). Hivyo vifuko hujaa hewa wakati wa kuruka, basi huzidi hao ndege kuwa wepesi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, hawakutazama washirikina kuwaangalia ndege walivyoendeshwa na kuwezeshwa kuruka angani, baina ya mbingu na ardhi, kwa amri ya Allah Mtukufu? Hakuna anayewazuia wasianguke isipokuwa Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kwa kuwa amewaumbia mbawa na mikia na Akawawezesha kuruka. Hakika katika huko kuendeshwa na kuzuiliwa kuna alama za ushahidi kwa wale wanaoziamini dalili za uwezo wa Allah Mtukufu
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net