Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nahl
Sura ya 16

An-Nahl

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 79

أَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَى ٱلطَّيْرِ مُسَخَّرَٰتٍ فِى جَوِّ ٱلسَّمَآءِ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا ٱللَّهُ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ 79

{79} Yaani, kwa sababu wao ndio wanaonufaika na Ishara za Mwenyezi Mungu, wanaotafakari katika yale yaliyowekewa ishara hizo. Na ama wengineo, hao hutazama kwao ni pumbao tu na kughafilika. Na ishara iliyo ndani yake ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaumba na umbile linalofailia kupaa, kisha akawatiishia hewa hii nyembamba, kisha akawekea ndani yake nguvu nyingi za kufanya harakati zilizowawezesha kufanya hivyo. Na huu ni ushahidi juu ya hekima yake, elimu yake pana, utunzaji wake wa kiungu kwa viumbe vyake vyote, na ukamilifu wa uwezo wake, yeye Mwingi wa baraka, Mola Mlezi wa walimwengu wote.