An-Nahl
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۢ بُيُوتِكُمْ سَكَنًا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ ٱلْأَنْعَـٰمِ بُيُوتًا تَسْتَخِفُّونَهَا يَوْمَ ظَعْنِكُمْ وَيَوْمَ إِقَامَتِكُمْ ۙ وَمِنْ أَصْوَافِهَا وَأَوْبَارِهَا وَأَشْعَارِهَآ أَثَـٰثًا وَمَتَـٰعًا إِلَىٰ حِينٍ 80
{80} Yeye Mtukufu anawakumbusha waja wake juu ya neema zake, na anawataka kuzishukuru na kuzitambua. Alisema, "Na Mwenyezi Mungu amewajaalia majumba yenu yawe ni maskani yenu" katika nyumba, makasri na mfano wake, ambazo zinawahifadhi kutokana na joto na baridi, na zinawasitiri nyinyi na wana wenu, na vitu vyenu. Na mnajitengenezea katika maskani hayo nyumba na vyumba. Nyumba ambamo mna manufaa na masilahi yenu na faida zinginezo zinazoonekana. "Na amewajaalia kutokana na ngozi za wanyama;" ima kutokana na ngozi yenyewe, au vile vinavyomea kutokana nayo kama vile sufi, nywele, na manyoya "nyumba mnazoziona nyepesi" katika safari na maeneo mnayoshukia ambayo hamkusudii kuishi hapo, ili yawazuie kutokana na joto, baridi, na mvua, na yanazuia mizigo yenu kutokana na mvua. "Na" amewajaalia "kutokana na sufi zao, na manyoya yao, na nywele zao, mnafanya vyombo." Na hivyo vinajumuisha kila kinachotengenezwa kutokana navyo kama vile vyombo, matandiko, mavazi na vitu vinginevyo. "Na furaha kwa muda;" yaani, mnafurahia kwavyo katika dunia hii na mnafaidika nayo. Basi hivi ni katika vitu ambavyo Mwenyezi Mungu amewafanya waja wake kuvitengeneza na kuvifanya.