Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 80

An-Nahl 16:80

النحل

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۢ بُيُوتِكُمْ سَكَنًا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ ٱلْأَنْعَـٰمِ بُيُوتًا تَسْتَخِفُّونَهَا يَوْمَ ظَعْنِكُمْ وَيَوْمَ إِقَامَتِكُمْ ۙ وَمِنْ أَصْوَافِهَا وَأَوْبَارِهَا وَأَشْعَارِهَآ أَثَـٰثًا وَمَتَـٰعًا إِلَىٰ حِينٍ

Maana

Na Mwenyezi Mungu amewajaalia majumba yenu yawe ni maskani yenu, na amewajaalia kutokana na ngozi za wanyama, nyumba mnazoziona nyepesi wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu. Na kutokana na sufu zao, na manyoya yao, na nywele zao, mnafanya vyombo na mapambo ya kutumia kwa muda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu amekujaalieni majumba yenu yawe ni maskani yenu, na amekujaalieni kutokana na ngozi za wanyama nyumba mnazo ziona nyepesi wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu. Na kutokana na sufi zao na manyoya yao na nywele zao mnafanya matandiko na mapambo ya kutumia kwa muda. [80]

[80] Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ndiye aliye kujaalieni mkaweza kusimamisha nyumba zenu ili ziwe maskani yenu. Na akakujaalieni kutokana na ngozi za ngamia, na ng'ombe, na kondoo na wanyama wengineo mkafanya mahema ambayo ni kama nyumba za kukalia, na mkihama nayo mnapo safiri na mnapo tua. Na kutokana na sufi zao, na nywele zao, na manyoya yao, mkafanya matandiko ya kutumia hapa duniani mpaka itakapo fika ajali yenu ya kuondoka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu, Aliyetakasika na sifa za upungufu, Amewapatia nyinyi mapumziko na utulivu kwenye nyumba zenu pamoja na watu wenu mkiwa mijini, na Amewapatia nyinyi mahema ya ngozi za wanyama howa, ambayo ni sahali kwenu mkiwa safarini, na ambayo ni sahali kwenu kuisimamisha pale mkaapo baada ya safari, na Amewapatia nyinyi kutokana na manyoya ya kondoo, manyoya ya ngamia na manyoya ya mbuzi vyombo vya matumizi yenu ya kuvaa, kujifunika, kutandika na pambo la nyinyi kujifurahisha kwalo mpaka kipindi kilichotajwa na wakati ujulikanao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net