Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 81

An-Nahl 16:81

النحل

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَـٰلًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلْجِبَالِ أَكْنَـٰنًا وَجَعَلَ لَكُمْ سَرَٰبِيلَ تَقِيكُمُ ٱلْحَرَّ وَسَرَٰبِيلَ تَقِيكُم بَأْسَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعْمَتَهُۥ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْلِمُونَ

Maana

Na Mwenyezi Mungu amewafanyia vivuli katika vitu alivyoviumba, na amewafanyia maskani milimani, na amewafanyia nguo za kuwakinga kutokana na joto, na nguo za kuwakinga katika vita vyenu. Ndivyo hivyo anavyowatimizia neema zake ili mpate kujisalimisha kwake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu amekufanyieni vivuli katika vitu alivyo viumba,na amekufanyieni maskani milimani, na amekufanyieni nguo za kukingeni na joto, na nguo za kukingeni katika vita vyenu. Ndio hivyo anakutimizieni neema zake ili mpate kut'ii. [81]

[81] Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni miti na vitu vyenginevyo vya kukupeni vivuli kukulindeni na taabu ya joto, na amekufanyieni mapango milimani, nanyi mkafanya humo maskani kama nyumba. Pia amekuumbieni nguo za sufi na pamba na kitani na vyenginevyo, ili kukuhifadhini na joto la jua, na nguo za chuma za kukulindeni katika vita na adui zenu. Kama alivyo kujaalieni hayo, basi kadhaalika amekutimizieni neema zake kwa kukupeni Dini iliyo simama sawa, ili mpate kuifuata amri yake, na mumsafie ibada Yeye tu si na mwenginewe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Amewapatia miti na vinginevyo vya kuwaletea vivuli, na amewafanyia kwenye majabali na pango sehemu za kuhamia mnapohitajia, na Amewafanyia nguo kutokana na pamba na sufi na vinginevyo za kuwahifadhi na joto na baridi, na Amewaumbia chuma cha nyinyi kujikinga na silaha za kudunga za maadui wenu na madhara yao katika vita vyenu na wao. Kama vile Alivyowaneemesha kwa neema hizi, atawakamilishia neema Zake kwenu kwa kuwafafanulia wazi Dini ya haki, ili mjisalimishe kwa amri ya Allah Mtukufu, Peke Yake, na msimshirikishe na kitu chochote katika ibada Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net